Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:30 pm

NEWS: TAKUKURU YAMBURUZA KORTINI MKURUGENZI WA MIPANGO TAKUKURU

Dar es salaam: Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imemfikisha mahakamani Mkurungenzi wa Mipango Kulthum Mansoor wa Taasisi hiyo akidaiwa kughushi nyaraka mbalimbali na kujipatia fedha taslim kwa njia ya udanganyifu zaidi ya BILIONI 1 na MILIONI 400 kutoka kwa watumishi wa TAKUKURU kwa madai ya kuwauzia viwanja.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Machi 29, 2019 Naibu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU amesema Kulthum alilipwa fedha kwa utaratibu waliokubaliana, watumishi waliokamilisha malipo walianza kuona dalili za kudanganywa baada ya kutokabidhiwa Hati inayoonyesha umiliki halali wa viwanja walivyokuwa wakinunua na alipoulizwa alisema vina mgogoro

"Uchunguzi uliofanywa ulibaini viwanja vilivyoahidiwa kuuzwa vilikuwa zaidi ya 300, fedha alizolipwa Bi. Kulthum ni zaidi ya Bil. 1 na Mil. 400, Mtuhumiwa alijipatia fedha nyingine zaidi ya Mil. 200 alilipwa kama gharama kwa ajili ya hati" Naibu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU

"Kulthum alijiunga na TAKUKURU na kuwa ktk nafasi ya Mkurugenzi wa Mipango October 2009 akiwa amehamishiwa kutoka Tume ya Kurekebish Sheria" na "TAKUKURU ilimsimamisha kazi rasmi Bi. Kulthum Mansoor tangu mwezi March tarehe 8 mwaka 2018" amesema Naibu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU

Jana March 28, 2019, wakati Rais Magufuli akikabidhiwa ripoti ya TAKUKURU ya mwaka 2017/2018 Rais alimtaji mtu huyo kuwa anatuhuma za kuwadhulumu viwanja baadhi ya wafanyakazi wenzake wa TAKUKURU.