- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAKUKURU KUMBURUZA MAHAKAMANI MKUU WA TAKUKURU KINONDONI DAR
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania (Takukuru) imesema inakusudia kuwakamata watumishi wake watano akiwamo mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Teddy Mjangira ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Taarifa hiyo hiyo imetolewa leo Alhamisi Machi 26, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo baada ya kuhojiwa na Gazeti la Mwananchini.
Mbungo amesema watumishi hao kwa pamoja wanatuhumiwa kumfanyia uchunguzi mtumishi wa umma ambaye hakuwa na kosa.
Amesema hatua hiyo ilimsababishia usumbufu usiokuwa wa lazima.
“Tutawakamata, tutawaweka ndani na tutafanya uchunguzi kujua hasa nini kilitokea. Lakini niseme tu kuwa utumishi wa umma unahitaji kuwa na maadili na nidhamu na tuna imani mkuu wetu (wa Kinondoni) amepotoka,” amesema Mbungo
Mapema leo Alhamisi asubuhi, Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati akipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2018/19 na ya Takukuru ya mwaka 2018/19 Ikulu ya Chamwino, Dodoma aliipongeza taasisi hiyo ya ukaguzi huku akigusia watumishi hao wa Kinondoni bila kufafanua zaidi.
Kutokana na utendaji mzuri wa Takukuru, Rais Magufuli amemdhibitisha Brigedia Jenerali John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.