Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:39 pm

NEWS: TAKRIBANI WANAHABARI 95 WAMEUWAWA MWAKA JANA

Ikiwa Ijumaa wiki hii dunia nzima inaadhimisha siku ya kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Takwimu zinasema kuwa jumla ya waandishi wa habari 95 waliuawa mwaka 2018 na hii ni kwa mujibu wa shirikisho la kimataifa la wanahabari Duniani IFJ.

Image result for press conference

Siku hii ya wanahabari inaadhimishwa huku dunia ikishuhudia waandishi wa habari wakiendelea kuuawa, kupokea vitisho, kuteswa , kupotezwa na hata kutekwa kwenye maeneo mbalimbali duniani.

Related image

Ni mwaka mmoja sasa na kidogo umetimia tangu mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda alipotoweka katika eneo la Kibiti Mkoani Pwani.

Maswali yanayosalia katika kipindi cha siku zaidi ya 360 ni moja nalo ni wapi alipo mwanahabari huyo na ikiwa yu hai au ameuawa na watesi wake wana shabaha ipi licha ya serekali yetu ya Tanzania kupitia waziri mwenye dhamana ya habari Dkt Harrison Mwakyembe kupiga marufuku watu wanaotaka kuhoji juu ya kupotea kwa mwanahabari huyu.

Gwanda alikuwa akiandikia gazeti la Mwananchi na alitekwa Novemba 21 mwaka 2017 akiwa katika eneo la Kibiti Mkoani, Pwani.

Tangu kutekwa kwake, vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania vimeripoti kwa kina tukio hilo huku pia wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania wakipaza sauti wakitaka uchunguzi ufanywe kuhusu kutoweka kwa mwanahabari huyo.

media

Hata hivyo, serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya ndani, Kangi Lugola imekuwa ikisisitiza kwamba inafanya uchunguzi wa visa vyote vya kutoweka kwa watu wakiwemo wanahabari, kupitia Jeshi la Polisi

Bara la Afrika ni miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa hatari zaidi kwa waandishi wa habari kufanya kazi huku ikishuhudiwa vyombo vingi vikifungwa au kupokea vitisho.

Kwa upande wake shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka RSF, lenyewe linaonya dhidi ya Serikali zinazominya uhuru wa habari, likitolea mfano hali inayoshuhudiwa nchini Burundi.