- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAHADHARI YA KUNYESHA KWA MVUA KUBWA NCHINI
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini Tanzania.
Mvua zinazoendelea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi pamoja na kanda ya kati zinatarajiwa kusambaa katika maeneo mengine ya nchi. Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda mvua na kusogea zaidi katika maeneo hayo. .
Hivyo, tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa kwa siku ya kesho tarehe 21/12/2019 inatolewa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma, Singida, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. .
Aidha, kwa tarehe 22/12/2019 vipindi hivyo vya mvua kubwa vinatarajiwa kupungua. Hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa Angalizo la mvua kubwa.