Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:41 pm

NEWS: TAARIFA YA KUJIUZULU KWA RAIS WA BRAZIL

Rio de Janeiro: Rais wa Brazil Bw.Michel Temer leo amekumbana na maandamano makubwa kuwahi kutokea katika kipindi chake akiwa madarakani, maandamano hayo yanayo mtaka Bw. Temer kujiuzulu kufuatia kashfa ya Rushwa inayo mkabili kwa sasa, hapo awali maandamano ya kumtaka Bw Temer kujiuzulu yalikuwepo ya wastani, sasa baada ya hivi karibuni Mahakama Kuu kutoa amri ya kumchunguza kutokana na kuhusishwa kwake na rushwa ndio imezusha maandamano makubwa nchini Brazil.


Maandamano makubwa yalifanyika katika miji tofauti tofauti hasa miji ya Sao Paulo na Rio de Jenairo, ambapo mamia ya waandamanaji walitembea kandoni mwa fukwe za bahari huku wakiimba na wengine wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa ''Temer Nje!''.


Hasara ya maandamano hayo yamesabaisha kushuka kwa sarafuya nchi hiyo na pia hasara kwenye soko la hisa. Mzozo huu mpya sasa umesababisha kuzorota kwa mageuzi kadhaa yaliyowekwa kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi wake ulioporomoka.