Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:49 pm

NEWS: TAARIFA YA HALI YA LISSU MPAKA SASA, WAKILI WAKE AONGEA

Dar es salaam: Mbunge wa singida mashariki na Rais wa chama cha mawakili Tanzania(TLS) Tundu Lissu Bado anaendelea kushikiliwa na Polisi mpaka hivi sasa, Lissu alikamatwa jana Uwanja wa ndege wa Julia's Nyerere Dar es salaam na maafi wa polisi na kumtaka waende nae kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi,

Leo kupitia wakili wake Fatma Karume ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Mzee karume amesema kuwa Polisi bado wanamshikilia Mh Tundu Lussi na wamekataa kumpa dhamana kwa sababu bado wako kwenye uchunguzi,“Watu wa Juu ndiyo wataamua!” ALIJIBIWA Fatma



Fatma aliwasilisha ujumbe wa Lissu baada ya kuongea nae, kuwa watu wasikate tamaa mapambano bado yanaendelea na yeye yupo okey.

Jana Fatma baada ya kukosa dhamana ya mteja wake aliongea haya

"Nimekwenda kumwakilisha mteja wangu Tundu Lissu Kituo Kikuu cha Polisi “Dar Es Salaam Central Police” jioni ya leo (jana Alhamisi). Anashikiliwa kwa makosa ya uchochezi kinyume na kifungu cha 390 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code). Nimewauliza Polisi wanadhani Tundulissu amemchochea nani na ni kosa gani la jinai ambalo mtu huyo aliyechochewa amelitenda. Jibu nililopokea ni “Bado Tunachunguza!” Nimewataka Polisi wampe dhamana, wamekataa kufanya hivyo kwa maelezo kuwa “Watu wa Juu ndiyo wataamua!” Kwa hiyo Mbunge na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika anatumia usiku mzima akiwa selo kwa kutuhumiwa kufanya uchochezi kwa watu wasiojulikana na akiwachochea watu hao wafanye makosa yasiyojulikana na ambayo yanachunguzwa. Hii haikubaliki, ni matumizi mabaya ya mamlaka ya kukamata ambayo polisi wamepewa na ni kitendo ambacho kinapaswa kupingwa na kulaumiwa na Watanzania wote!"