- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SUMAYE "HUU UTARATIBU WA KUCHANGIA SEREKALI KUPITIA MISIBA UMEANZA LINI?"
Dar es salaam: Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Mh. frederick sumaye amelaani utaratibu uliofanywa na serekali kupitia ofisi ya mkoa wa Arusha kwa kuhamisha fedha za msiba na kupeleka kwenye matumizi mengine, kama utakumbuka Baada ya msiba wa Lucky Vicente zilichangwa fedha na baada ya hapo watu wakatumia fedha hizo kwa ajili ya kuaga maiti na kufanyia mazishi.
Sumaye alitolea mfano wa wahanga wa Tetemeko kule mkoani kagera ambapo zaidi ya Tsh bilioni 4.7 zilitumika kukarabati miundominu. "Tujuavyo sisi huwa tunachangia kuwasaidi waliopatwa na tatizo, sasa huu utaratibu mya wa kuichangia serekali kupitia misiba na majanga umeanza lini na nichombo gani kimeupitisha utaratibu huu" alisema Summaye.
Aliendelea kwa kusema kuwa "Niabu kwa serekali kufanya hivyo, Serekali iache kutumiamabavu kwa kuchukua michango ya watu kwa kutumia kinyume na wachangiaji walivyo kusudia" watanzania wapenda amani na wapenda haki laazima tulaani kitendo hicho cha uwonevu na ukatili pia kinakiuka haki za binaadamu"
Pia sumaye aliongelea swala la kukamatwa na kuwekwa korokoroni kwa Meya na wenzake ambao walikuwa wanawasilisha michango kwa wafiwa "mtindo wa kutesa watu wasio nahati kwa sababu ya kisiasa ni chachu ya machafuko katika nchi na amani hii tuliyo nayo ikitoweka hakuna atakae pona" alimalizia Sumaye