Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:43 am

NEWS: SULUHU "TUNAPOTEZA WANAWAKE 556 KWA TATIZO LA UZAZI"

Dodoma: TANZANIA inapoteza zaidi ya wakinamama 556 kutokana na vifo vya uzazi katika kila wakina mama 100,000 wanaokwenda kujifungua kwa mwaka pia kifo cha mama na mtoto kinachotokana na uzazi, kijadiliwe ndani ya masaa 24 katika vituo au hospitali husikia kwa lengo la kubaini chanzo cha kifo na kutoa taarifa na kuchukua hatua stahiki .


Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ukumbi wa chuo cha mipango mjini hapa kwenye maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani Makamu wa Rais amesema hali hiyo inaonyesha kuongezeka kwa vifo hivyo ikilinganishwa na mika ya nyuma.

Amesema katika kipindi cha nyuma vifo vilikuwa ni wakina mama 432 katika kila mwaka wakina mama 100,000 wanokwenda kujifungua.

‘’Ni jambo la kusikitisha kuona tunarudi nyuma kwani Tanzania tulishapiga hatua katika kuzibiti vifo hivyo na kutimiza goli namba nne na tano la malengo ya milenia’’ amesema Samia.

Amesema vifo hivyo vinaweza kuepukika iwapo wakina mama hao watahudhuria kliniki na kuhudumiwa na wahudumu wenye ujuzi na uzoefu.
Samia amesema moja ya sababu kubwa ya vifo hivyo ni pamoja na kutopatikana kwa huduma sahihi wakati wa kujifungua.


Amesema serikali inakusudia kuhakikisha kuwa asilimia 50 ya vituo vya afya nchini vinavyomilikiwa na serikali vinatoa huduma kamili ya uzazi na dharura ifikapo 2020.
Makamu amesema kwa sasa ni asilimia 21% tu ya vituo 473 vinavyomilikiwa na serikali ndiyo vinatoa huduma ya upasuaji na ili kuifikia asilimia hiyo 50 tayari serikali imechukua hatua ya kuvikarabati vituo vya afya 8 katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mara na Mwanza.


Makamu amesema vituo vya afya 145 vipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji ili kuweza kutoa huduma za dharura zxa uzazi ikiwemo upasuaji.


“ Ni matarajio yetu kuwa ifikapo desemba mwaka huu vituo hivyo vitakuwa vimekamilika na vitakuwa na chumba cha upasuaji, maabara ya damu katika mikoa mitano.
Kwa upande wa idadi ya wakina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya , Makamu wa Rais amesema kumekuwa na mabadiliko ya idadi ya akina mama kutoka asilimia 51 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 64% mwaka 2015/16.''


Awali Rais wa Chama cha Wauguzi Nchini Feddy Mwanga amesema kuna umuhimu wa kutenganisha elimu ya ukunga na uuguzi.


Amesema endapo elimu ya ukunga itatengwa pekee yake na kufundishwa kwa kina kutaweza kuzalisha wakumnga ambao wamebobea katika fani hiyo.
“Tupo tayari kushirikiana na Wizara katika kutengeneza mitaala hiyo nia ni kupunguza vifo vya wakina mama na watoto.


Pia amesema kumekuwa na matatizo mbalimbali yanayowagusa wakunga ikiwemo vitendea kazi..