- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SULUHU AWATAKA VIJANA WA SCAUT KUFANYA KAZI KWA KUJIAMANI ILI KUJENGA TAIFA LA VIJANA WEMA
DODOMA: RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JOHN MAGUFULI amekiagiza Chama Cha Scaut nchini kujikita zaidi katika kusisitiza malezi na makuzi ya vijana,ujasiri,ukakamavu na uzalendo ili kuendeleza mambo yaliyoasisiwa na chama hicho tangu kuanza kwake.
Akifungua sherehe za miaka 100 ya uskauti Tanzania kwa niaba ya rais ambazo Kitaifa zilifanyika jana mjini Dodoma makamu wa rais SAMIAH SULUHU HASSAN alisema mambo hayo kwa sasa yanahitaji kusisitizwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwa kuwa taifa linakabiliwa na mmomonyoko wa maadili kwa vijana.
Alisema rais kama mlezi wa chama hicho atajisikia vyema kufanya kazi nao katika kuwajenga vijana katika maarifa,kuwalea katika misingi ya kizalendo,kuwaelekeza kujiamini ili kuweza kujenga Taifa la vijana wema inavyowezekana.
Katika hotuba hiyo ya rais iliyosomwa na makamu wa rais Amewapongeza na kuwashukuru marais wastaafu waliotangulia ambao walikuwa walezi wa skauti kabla yake na kusema kwa hakika wamea askauti katika nyakati za raha na changamoto lakini wamelea KWA US=TASHI MKUBWA KWA uzalendo na kujiamini na kwa huruma na kutekeleza dhima ya chama kwa uhodari mkubwa.
Akisisitiza baada ya kumaliza kusoma hotuba hiyo makamu wa rais pamoja na mambo mengine amewataka viongozi wa skauti na girl guides kujikita katika kuangalia katiba ili waone namna ya kuwalea vijana hao kwa pamoja.
Sherehe hizo ziliambatana na utoaji wa tuzo na nishani kwa rais MAGUFULI kama mlezi wa chama hicho kwa sasa ambayo ilipokelwa na makamu wa rais kwa niaba yake na kwa marais wote wastaafu kama ishara ya kutambua mchango wao mkubwa wa kulea chama hicho wakiwa viongozi.
Wakizungumza marais hao wastaafu akiwemo rais wa awamu ya pili mzee Alli Hassan Mwinyi,rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete,rais mstaafu wa sita wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume na waziri mkuu mstaafu SALIM AHMED SALIM kwa nyakati tofauti wameeleza namna walivyokilea chama hicho.
Kwa upande wake rais wa Chama Cha Skauti nchini ambaye ni waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi profesa JOYCE NDALICHAKO aliwataka skauti kufanya kazi kwa bidii na kuenzi misingi imara iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili.
Awali Kamishna mkuu wa chama hicho ABDULKARIM SHAA ameainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ofisi kwa ajili ya makamishna wa skauti mkoa na wilaya ,baadhi ya wazazi kutowaruhusu watoto wao kujiunga na skauti na baadhi ya viongozi kuona chama hicho ni cha kisiasa ilhali sio kweli.
Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na wake wa marais wastaafu,wawakilishi kutoka nchi za Comoro,Kenya,Uganda na Rwanda ambapo mbali ya kutolewa tuzo kwa marais wastaafu pia imetolewa tuzo kwa makamu wa rais SAMIAH SULUHU HASSAN,makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara ndugu PHILIP MANGULA,waziri mkuu msaafu MIZENGO PINDA na waziri mkuu mstaafu SALIM AHMED SALIM.
Chama Cha Skauti kilianza mwaka 1917 kabla ya Uhuru wa Tanganyika kikiwa na wanachama 19 ambapo kwa sasa kina wanachama zaidi ya laki 4 lengo likiwa ni kuchangia maendeleo ya vijana kufikia utimilifu wa vipaji vyao vya kimaumbile,kiakili,kijamii na kiroho.