Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:31 am

NEWS: SULTAN WA OMAN AFARIKI DUNIA KWA KANSA

Sultani wa Oman Qaboos bin Said aliyeitawala nchi hiyo kwa karibu nusu karne amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79, shirika la habari la taifa limeripoti.

Qaboos ambaye amekuwa sultan wa Oman tangu mwaka 1970 baada ya kumpindua baba yake, amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu na inaaminika alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo.

Kufuatia kifo chake serikali imetangaza siku tatu za maombelezo ya taifa na bendera zitapepea nusu mlingoti kwa muda wa siku 40.

Qaboos aliyeata elimu yake nchini Uingereza alifanya maguéuzi makubwa nchini Oman, taifa ambalo wakati akichukua madaraka lilikuwa na shule tatu pekee na sheria kandamizi zilizopiga marufuku nishati ya umeme, redio, miwani na hata matumizi ya miavuli.

Chini ya utawala wake Oman ilikuja kufahamika kuwa eneo linapendelewa zaiid na watalii na taifa kiungo kwenye eneo la mashariki ya kati likisaidia marekani kuwaokoa wanadiplomasia wake waliokamatwa mateka nchini Iran na Yemen na hata kuwakaribisha maafisa wa Israeli wakati huo huo akipinga ukaliaji wa mabavu ardhi ya wapalestina.

Kifo cha sultani Qaboos kinatishia kuwepo wasiwasi wa kutokea machafuko kwenye taifa hilo la pembezoni ya rasi ya bara arabu lenye kiasi raia milioni 4.6.

Sultani Qaboos ambaye hakuwa na mke wala watoto hakutaja hadharani mrithi wake.

Kulingana na katiba ya Oman familia ya sultani inapaswa kumtaja mrithi wa kiti hicho ndani muda wa siku tatu tangu kinapotangazwa kuwa wazi.

Iwapo familia itashindwa kuafikiana kuhusu jina la yule anakayechukua wadhifa huo, mtu aliyeteuliwa na Qaboos kupitia barua kwenda kwa familia yake ndiye atakuwa mrithi wa kiti cha usultani.

Katiba ya Oman inameanisha kuwa sultani anapaswa kuwa sehemu ya familia ya kifalme, muumini wa dini ya kiislamu, mtu mzima, timamu na mtoto halali wa wazazi waislamu wa Oman.