- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: STENDI YA UBUNGO KUHAMIA KIBAMBA
Dodoma: SERIKALI imesema hadi sasa tayari halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa serikali za Mitaa (LAPF) wameazisha kampuni ya ubia ya mzizima Propeties Limited ambayo itahusika na usimamizi na uendeshaji wa shughuli za kituo kila siku.
Hayo yalielezwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jaffo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Ubungo,Said Kubenea (Chadema).
Katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua Serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza ahadi katika utekelezaji wa kuhamisha kituo cha mabasi cha ubungo.
Pia alitaka kujua mradi wa kuhamisha kituo cha mabasi unatarajia kutumia kiasi gani cha fedha.
“Serikali ilihaidi kuhamisha kituo cha mabasi cha ubungo kukipeleka eneo la mbezi jimbo la kibamba lakini mpaka sasa jambo hilo halijatekelezwa.
“Je serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza ahadi hiyo,je mradi huo wa kuhamisha kituo cha mabasi unatarajia kutumia kiasi gani cha fedha” amehoji Kubenea.
Akijibu swali hilo Jafo alisema hadi sasa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na mfuko wa Hifadhi ya jamii wa serikali za mitaa (LAPF) wameanzisha kampuni ya ubia ya Mzizima Properties Limited ambayo itahusika na usimamizi na uendeshaji wa shughuli za kituo za kila siku.
kazi inayoendelea ni kumtafuta mtaalam mshauri kwa ajili ya kuthibitisha usanifu wa mwishowa kina wa mradi ili kumpata mkandarasi wa ujenzi wa mradi.
Amesema gharama za ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi cha Mbeizi Luis zimekadiriwa kuwa sh. bilioni 28.71 zitazotolewa kwa ushirikiano wa halmashauri ya jiji na mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Aidha amesema gharama halisi zitajulikana baada ya usanifu wa kina utakaofanywa na mtaalam mshauri.