- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA WA BUNGE WA VENEZUELA AONDOLEWA MADARAKANI NA HATOWEZA KUGOMBEA TENA
Spika wa Bunge la Venezuela Juan Guaido, ambaye pia ndio kiongozi wa upinzani,anayepigiwa upatu na mataifa ya Ulaya na Marekani ameondolewa kwenye nafasi yake ya Uspika wa Bunge na hatoweza kushikilia nafasi yoyote nyingine anayepewa mtu aliyechaguliwa, kwa muda wa miaka 15 kwa madai ya rushwa, mamlaka nchini Venezuela imesema.
Mkaguzi Mkuu wa serikali Elvis Amoroso, anayehusika na masuala ya uwazi katika utawala nchini Venezuela, ameamua "kuzuia nafasi zote anazoweza kusimamia mtu aliyechaguliwa kwa mwananchi (Juan Guaido) kwa kipindi cha juu kilichotolewa na sheria" Amoroso ametangaza kwenye televisheni ya serikalii katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Alhamisi jijini Caracas.
Kwa mujibu wa Elvis Amoroso, Juan Guaido hajatoa maelezo kuhusu gharama za safari zake za nje ya nchi na fedha anazopata kutoka nchi nyingine. "Alifanya safari zaidi ya 91 nje ya nchi kwa gharama kubwa kuliko bolivar milioni 570 (sawa na dola za Marekani 168,000 kwa bei ya sasa) bila kutoa maelezo wapi fedha hizo zimetoka," amesema Mkaguzi Mkuu wa serikali, akiongeza kuwa Juan Guaido "alitumia mamlaka aliyopewa na wananchi na kufanya vitendo na serikali za kigeni ambazo zimewatia hatarini wananchi wa Venezuela.
Juan Guaidó amefutilia mbali adhabu hiyo, "yeye si mkaguzi wa serikali" amesema, "Bunge pekee ndio halali ya kuteua Mkaguzi Mkuu wa serikali.