- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA WA BUNGE WA IVORY COAST AELEKEA KUJIUZULU
Kikao kisichokuwa cha kawaida cha bunge la Cote d'Ivoire kilitishwa Jana Ijumaa, Februari 8 katika hali ya kujadili hatima ya Spika wa bunge Guilluame Soro, ambayo inaelekea kuwa huenda angechukuwa hatua ya kujiuzulu jana Ijumaa.
Hatua ya kujiuzulu kwa Guillaume Soro ilitangazwa mwishoni mwa mwezi Januari na rais Alassane Ouattara. Wawili hao walikubaliana kuhusu suala hilo, baada ya Guillaume Soro kukataa kujiunga na chama kipya cha RHDP.
Suala hili la kujiuzulu kwa Guillaume Soro limekuwa gumzo mjini Abidjan. Spika wa Bunge na rais Alassane Ouattara walikutana angalau mara mbili tangu mwanzoni wa mwaka huu ili kujadili suala hilo la kujiuzulu kwenye nafasi ya spika wa bunge.
Alassane Ouattara mwenyewe alitamka mbele ya waandishi wa habari tarehe 28 Januari mwaka huu akisema kuwa: "Guillaume Soro atajiuzulu mnamo mwezi Februari, tumekubaliana, suala hilo limekwisha patiwa ufumbuzi.