Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:48 am

NEWS: SPIKA WA BUNGE WA CONGO ATIMULIWA

Kinshasa: Bunge la Kinshasa chini Congo limemtimua mwenyekiti wake Bw Roger Nsingi. kiongozi huyo wa kundi la zamani la waasi la MLC la Jean-Pierre Bemba, ambaye leo anatumikia katika chama cha MLC/Liberal, Roger anaongoza bunge hilo kwa miaka kumi na moja sasa.

Wabunge 39 kwa kauli moja walioshiriki kikao cha siku ya Alhamisi walipiga kura ya kufukuzwa kwa spika huyo.

Spika wa mkoa wa mji wa Kinshasa alikua akilengwa na mbunge Jolino Makelele kwa kumtuhumu spika huyo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma na kutowajibika kwa mamlaka yake.

Roger Nsingi hakushiriki katika kikao hicho kilichoamua hatima yake. Kutoshiriki kwa kiongozi huyo kwenye kikao ni kosa hubwa, kwa mujibu wa wabunge wa mkoa walishiriki kikao cha siku ya Alhamisi.

Roger Nsingi alichaguliwa mbunge wa mji wa Kinshasa kupitia tiketi ya chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba Gombo mwaka 2006, lakini alikihama chama hicho cha upinzani baada ya ku MLC kugawanyika.