Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:33 am

NEWS: SPIKA WA BUNGE LA TUNISIA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA TUNISIA WA MUDA

Bunge la Tunisia limemchagua Spika Mohamed Ennaceur kuwa kaimu rais wa nchi hiyo baada ya kifo cha rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo Beji Caid Essebsi kufariki dunia usiku wa kuamkia Jana Alhamisi.

Image result for Mohamed Ennaceur

Mohamed Ennaceur ataongoza Tunisia wakati wa kipindi cha mpito hadi uchaguzi mpya utaandaliwa.

media

Essebsi aliyekuwa na umri wa miaka 92 mpaka mauti yanamfika, aliingia madarakani mwaka 2014, miaka mitatu baada ya kuangushwa kwa utawala wa Zine El Abidine Ben Ali kupitia maandamano yaliyosababisha kuenea kwenye nchi nyingine za mashariki ya kati.

Licha ya kuchaguliwa kidemokrasia, Essebsi hakuwa na urahisi wa kuongoza nchi hiyo kutokana na mgawanyiko wa wanasiasa na hali tete ya uchumi na usalama.

Alikuwa kiongozi mkongwe zaidi duniani. Alilazwa hospitali Jumatano lakini maafisa hawakueleza kwanini alipelekwa kupokea matibabu.

Beji Caid Essebsi alilazwa hospitalini mwezi uliopita baada ya kukabiliwa na kile maafisa walichotaja kuwa hali mbaya ya afya.

Mapema mwaka huu, Essebsi alitangaza kwamba hatowania katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa Novemba.