Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:52 pm

NEWS: SPIKA WA BUNGE LA MAREKANI ACHANA HOTUBA YA RAIS TRUMP HADHARANI

Usiku wa Kuamkia leo Taifa la Marekani limeshuhudia Mpasuko mkubwa wa kisiasa mara baada ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump kususa kumpa mkono Spika wa Bunge la wawakilishi Nancy Pelosi naye Pelosi akamjibu kwa kuichana hotuba yake hadharani, hivi ni baadhi tu ya vitimbi vilivyodhihirisha mgawanyiko mkali nchini Marekani, wakati Trump alipotoa hotuba kuhusu hali ya nchi.

USA, Washington: Trump hält State of the Union Rede im Capitol (Getty Images/AFP/M. Ngan)

Tofauti na ilivyozoeleka kuwa hotuba ya rais wa Marekani kuhusu hali ya nchi ni muda wa maridhiano kisiasa, mazingira katika kikao cha Congress kilichowaleta pamoja wajumbe wa baraza la wawakilishi na maseneta yaliakisi mpasuko mkali wa kisiasa muda wote wa saa moja na dakika 18 wa hotuba ya Trump.

Zoezi zima lilianza vibaya pale Rais Trump alipokataa kuupokea mkono alionyooshewa na spika wa baraza la wawakilishi Bi Nancy Pelosi na kuuacha ukining'inia hewani. Na lilimalizika kwa hatua ya Pelosi kumjibu Trump mtindo wa jino kwa jino, alipochana vipande vipande nakala ya hotuba ya Trump aliyokuwa amekabidhiwa, mara tu Trump alipomaliza kuzungumza.

Wasaa wa kujitapa na kujigamba

Rais Trump ametumia sehemu kubwa ya hotuba yake kwa majigambo, ya namna alivyofanikiwa kuukarabati uchumi wa Marekani, na hadhi ya nchi hiyo, ambavyo amedai vilikuwa vimewekwa rehani na watangulizi wake.

USA, Washington: Trump hält State of the Union Rede im Capitol (Getty Images/AFP/M. Ngan)

''Miaka ya uozo wa kiuchumi imekwisha. Siku za Marekani kuhujumiwa kiuchumi na kukejliwa na mataifa mengine tumeziacha nyuma. Tumeipa pia kisogo mienendo ya kuvunja ahadi, na kutafuta visingizio vya kumomonyoka kwa uchumi, nguvu na fahari ya Marekani.'' Amesema Trump na kuongeza kuwa kwa miaka mitatu tu, ''tumevunjilia mbali mitazamo ya kwamba Marekani inadidimia.''

Masuala mengine aliyoyamulika Trump katika hotuba yake, ni mikubaliano ya kibiashara kati ya China, na mengine ya eneo huria la kibiashara katika nchi za Amerika Kaskazini, akisema hayo ni mafanikio makubwa ambayo yatarejesha maelefu ya viwanda nchini Marekani.

Amezungumzia pia sera za kupunguza kodi na kumaliza kuhusika kwa majeshi ya Marekani katika mizozo ya Mashariki ya Kati, kama ushahidi wa kutimiza ahadi alizozitoa kwa wapiga kura.

Ufa mpana kati ya Warepublican na Wademocrat

Hotuba yake ilishangiliwa mara kwa mara na wabunge wa chama chake cha Republican waliosimama kumpigia makofi, huku wademocrat wakibakia katika viti vyao, baadhi wakizomea, na wengine hata kutoka nje.