Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:54 pm

NEWS: SPIKA WA BUNGE LA LIBYA AOMBA MSAADA NCHI ZA KIARABU

Spika wa Bunge la Libya, Aguila Saleh, Jumatano asubuhi wiki hii, alikuwa ziarani Cairo. Mbele ya Bunge la jumuiya ya nchi za Kiarabu, alithibitisha kwamba vikosi vinavyoongozwa na Marshal Khalifa Haftar, vitaendeleza na harakati zao na hivi karibuni vitaingia Tripoli ili kuikomboa kutoka mikononi mwa wanamgambo.



Aguila Saleh pia ametoa wito kwa nchi za Kiarabu kutotambua tena serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli inayoongozwa na Fayez el-Sarraj.

Spika wa Bunge la Libya pia alitoa wito kwa nchi za Kiarabu kuingilia kati ili kukabiliana na Uturuki ambayo imeingilia kijeshi nchini Libya.

Aguila Saleh amebaini kwamba mikataba miwili iliyotiliwa saini kati ya Ankara na serikali ya Fayez el-Sarraj ni kinyume cha sheria, kwani hawajapata idhini ya Bunge.

Katika taarifa, Bunge la jumuiya ya nchi za Kiarabu limelaani uamuzi wa Uturuki wa kupeleka vikosi nchini Libya.