- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA WA BUNGE AWATISHIA WABUNGE
DODOMA: SPIKA wa bunge JOB NDUGAI amewahakikishia wabunge kuwa bunge sio dhaifu na kuwataka kujenga utamaduni wa kila mmoja kuheshimu mawazo ya mtu mwingine hata kama mawazo hayo hayawafurahishi.
Spika NDUGAI amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma baada ya kipindi cha maswali na majibu wakati akitoa ufafanuzi kuhusiana na kauli mbalimbali zilizotolewa jana bungeni na baadhi ya wabunge wa upinzani akiwemo mbunge wa Kibamba JOHN MNYIKA aliyesema kuwa bunge ni dhaifu.
Spika NDUGAI amesema ni lazima kama binadamu uwe na staha kwako uheshimu mawazo ya wenzako bila ya kuona mawazo yako ndio ya maana peke yake nayawenzio ni ya kijinga.
Akizungumzia wabunge waliopewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge amesisitiza kuwa yeye ndio spika anayeoongoza bunge na adhabu yao ipo pale pale hata kama wataenda wapi.
Ameahidi kuendelea kukemea na kuchukua hatua kutokana na tabia ambazo zinaenda kinyume na kanuni za bunge.