- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA WA BUNGE: ''ACHANI IMANI POTOFU''
DODOMA: SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,JOB NDUGAI amewataka wananchi, viongozi wa dini wakiwemo wanasiasa kuwa na umoja na kuacha kulumbana kuhusiana na hatua za Rais JOHN MAGUFULI ambazo amekuwa akizifanya katika kusimamia rasilimali za nchi kwa lengo la kuweza kunufaika nazo.
Spika NDUGAI ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati wa ibada ya uzinduzi wa harambee ya kuchangia jengo kubwa la kisasa ambalo litakuwa na ghorofa kumi kwaajili ya utoaji huduma mbalimbali za kidini na kijamii la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)linalotarajiwa kujengwa Mjini humo.
Aidha amebainisha kuwa haina haja ya wao kulumbana na badala yake wawe kitu kimoja katika kumuunga mkono Rais MAGUFULI kwa juhudi za kupambana na udhibiti wa rasilimali za nchi.
Katika hatua nyingine Spika huyo amewataka baadhi ya watu kuachana na imani potofu za mauaji ya vikongwe na maalbino na badala yake watende mambo yaliyo mema kama maandiko ya Mungu yanavyo agiza.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikiristo Tanzania (CCT)Mchungaji Canoni MOSES MATONYA akielezea juu ya jengo hilo ambalo litakuwa la kisasa amesema kuwa litaongeza kutoa sura nzuri ya Mji wa Dodoma hasa kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali.
Hata hivyo katika uzinduzi huo wa harambee ya kuchangia ujenzi huo ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini na wa kisiasa ambapo jumla ya Shilingi Milioni 147 laki nne na sabini na tano elfu zilipatikana huku fedha taslimu zikiwa ni sh Mil 60 na ahadi ni Sh Milioni 87 laki nne na sabini na tano elfu.