- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI: RUKSA WAPINZANI KUSOMA HOTUBA BILA KUHARIRIWA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kuazia sasa ni ruksa kwa viongozi wa upinzani bungeni kusoma hotuba zao bila kuhaririwa lakini akatoa tahadhari kuwa kutokuweka kwa maneno yanayoweza kusababisha migongano na mihimili mingine Njee ya Bunge.
Ndugai amesema hayo leo Alhamisi Aprili 25 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Godbles Lema ambayo ilisusiwa kusomwa jana na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Kauli ya Spika imekuja wakati katika mkutano huu wa 15 wapinzani wakishindwa kusoma hotuba mbili ikiwemo ya wizara ya habari ambayo msemaji wake Joseph Mbilinyi aondoe maneno kadhaa.
Kama utakumbuka Jana April 24 Msigwa alisema nafsi yake na wapinzani wenzake inamsuta kama angesoma maoni hayo aliyosema yamehaririwa kwa kiasi kikubwa na akaomba hotuba hiyo apelekewe waziri ili aisome. “Kabla ya kuendelea naomba nizungumzie jambo moja ambalo lilijitokeza jana na siku za nyuma, hizo hotuba za wenzetu wa upinzani kuna shida kidogo katika uandishi na wakati mwingine zinaleta matatizo makubwa, shida kuna watu wanaandika nje ya bunge na mawaziri vivuli hawazisomi wao wanafika na kusaini tu,” alisema Ndugai.
Akawaomba viongozi hao wa upinzani hasa kwa wale wanaosoma hotuba hizo kuwa makini na kuzisoma kabla ya kusaini ili wakibanwa makosa yawe ni juu ya wasomaji wenyewe. Kiongozi huyo wa Bunge ameagiza hotuba hizo zipelekwe bungeni kama zilivyo kawaida lakini akasema wataendelea kubishana hapo hapo bungeni.