- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI AWAKARIBISHA MBOWE NA MATIKO BUNGENI
Dodoma: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amemkaribisha Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko kuendelea na shughuli za kibunge.
Mbowe na Matiko leo Machi 12, 2019 wamewasili bungeni kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango anawasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Kabla Waziri Mpango hajaanza kuwasilisha taarifa yake katika ukumbi wa Pius Msekwa, Spika Ndugai alisema, "Kwanza nianze kwa kumkaribisha kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni (Mbowe) na mheshimiwa Esther Matiko kwa lugha ya kibunge tunasema walikuwa Mtera," amesema.
Machi 7, 2019 Mahakam Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliwarejeshea dhamana yao, baada ya kushinda rufaa waliyoikata wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu.
Awali Mbowe na Matiko walionekana wakikumbatiana na wabunge mbalimbali wa CCM na upinzani. Aidha, wakati Ndugai na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wanaingia wabunge wa CCM walianza kuimba wimbo wa chama chao, hali ambayo ilizua minong’ono miongoni mwa wabunge wakiwamo wa CCM