- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI AMTAKA CAG KUJIUZULU WADHIFA WAKE
Dar es salaam: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Professa Mussa Assad kujiuzulu nafasi yake kutokana na Bunge analoliongoza yeye kutokuwa na Imani nae.
Spika amesema kuwa kwa nchi zilizoendelea Bunge likishakuwa halina imani na wewe haupaswi kubaki ofisini “Kwakuwa Bunge lilisha azimia kutofanya kazi na mtu anaitwa Prof Juma Assad kwa kulidhalilisha Bunge, uamuzi huo ni halali na haungiliwi na mtu yeyote… nchi za wenzetu ikifika mahali Bunge limeonesha kutokuwa na imani nawe, unajiuzulu” amesema Spika Ndugai.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo April 14 jijini Dar es Salaam Ndugai amesema kuwa Profesa Assad amelinajisi bunge na anampa wakati mgumu Rais John Magufuli.
“Azimio la bunge ni halali …katika nchi za wenzetu bunge likikuwa halina imani na wewe hung’ang’ani unajiuzulu sisi hatumfundishi lakini anampa wakati mgumu Rais . ..aende kwa Rais amueleze rais kwamba aliteleza ..matusi hayo anayoyatoa kwa Bunge anamtukana kila mtu, Rais yupo mule, mawaziri wapo mule anautukana hadi mkono unaomlisha .. anauthubutu jasiri na ni shujaa lakini ushajaa wake ni wa Mbwa kung’ata anayempa chakula.”
Amesema kuwa bunge halijachukuziwa na Ripoti ya (CAG) kutokana na bunge halijaguswa na ripoti hiyo tatizo ni maneno aliyoyatumia CAG kuliita Bunge Dhaifu.
“Neno dhaifu kihasibu mkaguzi analitumia kwa taasisi anayoikagua na kuwatumia washika dau anaofanyia kazi na washika dawa hapa ni bunge kwa ajili ya wananchi anachosema serikali anaelekeza anapoelekeza anaogopa kusema yeye amewekwa na serikali kwa ajili ya kuangalia na kutuambia sisi hawezi tena kugeuka na kufanya alichofanya” amesema.
Amesema kuwa Profesa Assad ameendelea na msimamo wake wa kuliita Bunge Dhaifa pale alipohojiwa na Kamati ya Bunge na hata alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa jina hilo Bunge halipendezwi nalo lakini bado Profesa Assad analitumia “Hata katika maisha ya kawaida mtu anakuambia jina fulani silipendi anaendelea kukuita. Akaambiwa toa kamusi yako ya kiswahili neno lile ni neno lisilokuwa na heshima kwa bunge.
“Neno ambalo hatulipendi unalipenda jiite wewe na kuonyesha kuwa hatulipendi tukalichukulia hatua hata wenzetu . Kurudia na kuahidi utarudia tutakuita tena.” Amesema Ndugai.
Wakati huo huo Ndugai ametoa ufafanuzi juu ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bunge wiki iliyopita kuwa ni Maswali juu ya ripoti ile kwa maana Kamati za Bunge zitatoa ripoti kamili.