- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI AKATAA KUSOMWA KWA HOTUBA YA UPINZANI BUNGENI
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amekataa katu katu kusomwa kwa Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu bajeti ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa sababu imekiuka kanuni na taratibu za Bunge.
Uwamuzi huo ameufanya leo Aprili 1, 2020 Bungeni jijini Dodoma huku akisema kuwa awali alikuwa akiwaonya kambi hiyo kwa kuwataka kuondoa baadhi ya maeneo katika hotuba zao yanayokwenda kinyume na kanuni lakini kuanzia sasa atakuwa hafanyi hivyo na badala yake kuondoa hotuba nzima yenye maeneo yanayokiuka kanuni.
"Hotuba hii ya Kambi Rasmi ya Upinzani imejaa makosa karibia kila ukurasa, ina matumizi mabaya sana ya jina la Mhe. Rais na kulituhumu Bunge la 11. Nadhani wangeshirikiana kuiandika pamoja isingefika hapa, mimi siko hapa kutetea chochote" - amesema Spika Ndugai