- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI AFUTA UWAMUZI WA KUMSIMAMISHA MASELE KUHUDHURIA VIKAO
Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania Job ndugai ameamua kumfutia adhabu ya kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge Bunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele ambaye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilimkuta na hatia ya kugonganisha mihimili na utovu wa nidhamu.
Awali Kamati ya Haki, Maadili ilipendekeza Masele kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo Alhamisi Mei 23, 2019 baada ya kamati kuwasilisha mapendekezo hayo Spika Ndugai ameiomba Kamati hiyo kuhitimisha suala hilo la Makamu Rais wa BUNGE la Afrika kwa kutoijadili hoja iliyowasilishwa na kamati hiyo kutaka asimamishwe kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge
Ndugai ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 23, 2019 bungeni jijini Dodoma baada ya kamati hiyo kuwasilisha taarifa yake hiyo.
Kabla ya wabunge kuanza kuchangia maoni ya kamati hiyo, Ndugai alihitimisha jambo hilo kwa kutaka Bunge kumpuuza Masele. Mbali na kutaka kupuuzwa, Ndugai amesema amepokea ujumbe wa Masele kwamba anataka kuomba radhi.
Masele alikuwa akituhumiwa na Spika Ndugai kuwa alitoa tuhuma mbalimbali akidai Ndugai amewasiliana na Rais wa PAP ili amng’oe nafasi yake ya makamu wa Rais na ubunge wa Bunge hilo.
Masele pia ameikataa taarifa ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomkuta na hatia. Masele alihojiwa na kamati hiyo Jumatatu Mei 20, 2019 akituhumiwa na Ndugai kwamba amekuwa utovu wa nidhamu pamoja na kutoa maneno ya kugonganisha mihimili