Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:31 pm

NEWS: SPIKA ADAI KUIKAGUA OFISI YA CAG, ASEMA HAKUNA ATAKAYEBAKI

Dodoma: Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema ofisi yake imeikagua Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kwamba taarifa ya ukaguzi huo imekamilika huku akisema ‘katika masuala ya Ukaguzi hakuna anayebaki, wala anayejikagua mwenyewe'

“Nimeipokea, nimeshaipitia na taratibu zinanitaka niipeleke taarifa hiyo kwa PAC ili kuipitia na kuichambua. “Baada ya kukamilisha watawasilisha taarifa kwangu, katika masuala ya ukaguzi hakuna anayebaki, hakuna anayejikagua mwenyewe,” ameongeza Spika Ndugai

Akitoa taarifa hiyo leo Alhamisi Mei 16, 2019, bungeni, Spika Ndugai amesema kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi wa umma, hesabu za ofisi ya CAG zinakaguliwa na Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

“Hesabu za ofisi ya CAG zinapaswa kukaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na Bunge kupitia kamati ya kudumu ya PAC huwa inajukumu la kuteua mkaguzi wa ofisi hiyo.” “Kwa maneno rahisi, Bunge ndiyo tuna tafuta mkaguzi wa nje ambaye anakagua ofisi hiyo,” amesema Spika Ndugai.