- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SOKO LA MAKOROBOI LATEKETEA KWA MOTO
Mwanza. Soko la Makoroboi mkoani Mwanza limeteketea na moto na kuacha simanzi zito kwa wafanyabiashara wa eneo hilo lililo katika mwa jiji kutokana na bidhaa zao kuteketea na Moto huo.
Moto uliozuka majira ya saa 9 alfajiri ya leo Jumatano Februari 12, 2020 na unataarifiwa kuwa Moto huo uliowaka kwa dakika takribani 45 ulizimwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi, hakuna bidhaa zilizookolewa.
Muakilishi tulipiga stori na baadhi ya wahanga wa moto huo. "naitwa Juma Chuma yaani kaka moto huu mimi umeniacha kama yatima yaani kwasababu ndio ilikuwa sehemu yangu pekee ya kupatia riziki yangu"
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi amethibitisha amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vinaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo. Bidhaa za wafanyabiashara wadogo 159 zimeteketea huku mabanda 65 nayo yakiteketea.