Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:47 am

NEWS: SOKO LA HISI LA DAR ES SALAAM LAPOROMOKA MARA 21

Inaelezwa kuwa Mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka kwa zaidi ya mara 21 ndani ya kipindi cha wiki moja, huku sababu kubwa ikielezwa na wataalamu kuwa ni kushuka kwa shughuli za mauzo za soko hilo.

Kwamujibu wa Takwimu za DSE, zilizotolewa na kampuni ya udalali wa dhamana na mitaji na ushauri wa kiuwekezaji ya Zan Securities, zinaonyesha kuwa wiki inayoishia Agosti 23, 2019 mauzo yalikuwa TZS. 351.7m na yameshuka kutoka TZS. 7.5b katika wiki iliyoishia Agosti 16 mwaka huu.

Kwamujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa soko hilo Emmanuel Nyalali amesema katika wiki iliyoishia Agosti 23 mwaka huu, idadi ya mauzo ya hisa ilipanda hadi kufikia hisa milioni 3 ukilinganisha na wiki iliyotangulia ambapo hisa milioni 1.7 ziliuzwa sokoni

Nyalali amesema pia thamani ya mauzo ya hisa ilishuka kutoka TZS bilioni 7.50 katika wiki iliyopita mpaka kufikia TZS milioni 351.69.