November 25, 2024, 8:56 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM LAPOROMOKA TENA
Inaelezwa kuwa Biashara ya Hisa katika soko la Hisa la Dar es Salaam DSE imeporomoka pakubwa kwa wiki iliyopita baada ya kupungua kwa mauzo ya Hisa za Kampuni ya Bia nchini Tanzania TBL, ambayo ndio mchangiaji mkubwa katika thamani ya mauzo ya hisa kwenye soko hilo .
Meneja Miradi wa Soko hilo Emmanuel Nyalali akitoa taarifa ya mwenendo wa Biashara katika soko hilo, amesema kushuka kwa mauzo ya hisa za TBL kulichangiwa na kutokuwepo kwa ushiriki wa wawekezaji wa nje kwa wiki hiyo .
Kufuatia hali hiyo, wawekezaji wa ndani ndio waliochangia kwa asilimia 100 ya thamani ya mauzo yote ya hisa pamoja na asilimia 94.28 ya thamani ya manunuzi yote ya hisa. DSE imetoa wito kwa wawekezaji wa ndani hususan mifuko ya hifadhi ya jamii kuongeza uwekezaji wao kwenye soko hilo (DSE)