Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 6:41 pm

NEWS: SIRRO APIGA MARUFUKU POLISI KUJIHUSISHA NA SIASA

Arusha. Mkuu wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amewaonya polisi wote kutojihusisha na siasa kwa maelezo kuwa jukumu lao ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Amewataka askari polisi kupenda kazi yao zaidi, kujiamini kwa kusimamia sheria.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 21, 2019 alipotembelea nyumba za askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) zilizopo Njiro mjini Arusha.

Aidha Sirro amewaonya vikali askari polisi wenye tabia ya kuwauzia wenzao sare za jeshi hilo na kwamba iwapo watakaobainika watachukulia hatua kali za kisheria.

Amesema baadhi ya askari wenye tabia hizo wamekamatwa na kuwekwa mahabusu.

Sirro amesema nchini kuna askari zaidi ya 37,000 lakini uwezo wa kushona sare kwa ajili yao ni mdogo, kuahidi kila mkoa kuwa na cherehani kuondoa changamoto iliyopo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka viongozi wenzake kuwa wa kwanza kusimamia sheria ili kulirahisishia jeshi hilo utendaji wa kazi. Amebainisha kuwa polisi wanaposimamia sheria na kuchukua hatua baadhi ya viongozi wanalalamika jambo linaloathiri utendaji kazi wa polisI