Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:55 am

NEWS: SIRRO APIGA MARUFUKU KUMZUNGUMZIA LISSU

Mbeya: Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro ametaka KUFUNGWA mara moja kwa mjadala kuhusu kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.


Sirro ametoa agizo hilo leo akiwa ziarani jijini Mbeya wakati akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo amewaonya wanasiasa kuacha kuuendeleza na mjadala kuhusu nani aliyempiga Risasi mbunge huyo na waliachie jeshi la polisi lifanye kazi yake .

Simon Sirro


Sirro pia aliulizwa Kuhusu madai yaliyotolewa hivi karibuni na familia ya mbunge huyo kuwa jeshi hilo halina dhamira ya dhati ya kufanya uchunguzi, amesema kuwa hana cha kuwajibu kwa kuwa hataki malumbano na familia hiyo.

Lissu alishabuliwa Risasi mnamo tarehe 7 september mwaka huu akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na sasa mbunge huyo yupo Nairobi Kwa matibabu zaidi