Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:42 am

NEWS: SIMBACHAWENI APIGA KAMBI BANDARINI, ABAINI UPIGWAJI WA FEDHA

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Geogre Simbachawene imesema imebaini uwepo wa harufu ya rushwa na upigaji juu ya wanaosafirisha makontena ya chuma chakavu nje ya nchi kutopewi risiti halisi inayoonyesha ni kiasi gani cha mzigo unaosafirishwa jambo ambalo limeisababishia Serikali kukosa mapato kwa muda mrefu.

Waziri wa Mazingira na Muungano Tanzani, Geogre

Simbachawene ameyasema hayo leo Agosti 9, 2019 alipofanya ziara Bandari ya Dar es Salaam ili kukagua makontena yenye chuma chakavu ambayo hayaruhusiwi kusafirishwa nje ya Tanzania.

Waziri huyo mpya wa Mazingira ameongezea kuwa wanaosafirisha makontena ya chuma chakavu nje ya nchi hawana kibali kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) jambo ambalo wamekuwa wakisafirisha vyuma chakavu ambavyo haviruhusiwi.

“Serikali inapoteza mapato makubwa, watu wengi wanajua hii biashara haina mapato, kuna wengine wanasafirisha chuma chakavu na halisi ambayo haijaruhusiwa ikiwemo mataaluma ya reli, vyuma vya madaraja na nyaya za Tanesco hivyo chuma chakavu inayotakiwa kusafirishwa nje ya nchi ni aina ya dongo,” amesema

“Wanaofanya biashara hii siyo watu wadogo ni watu wakubwa na wanasafirisha vyuma chakavu ambavyo haviruhusiwi kusafirishwa na kila kontena moja likijaa thamani yake zaidi ya Sh200 milioni haitolewi risiti yeyote inasafirishwa tu,” amesema Simbachawene.

waziri huyo aliyechukuwa nafasi ya Januari Makamba amesema kuna fomu namba tatu ambayo anatakiwa kupewa mtu anayesafirisha chuma chakavu nje ya nchi inasaidia kujua imetoka wapi, anayesafirisha ni nani na inaenda wapi lakini hayo hayafanyiki watu wanasafirisha huku Serikali ikikosa mapato.