- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SIMBACHAWENE: 'AWATAKA WAKURUNGEZI WASIWE KIWANDA CHA KUZALISHA MADENI KWA SERIKALI'
Dodoma: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)George Simbachawene amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza kulipa madeni yote ya uhamisho ya walimu ifikapo Juni 30 mwaka huu.
Simbachawene ametoa agizo hilo Mjini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za mitaa wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Amebainisha kuwa endapo hawataekeleza agizo hilo wasije wakamlaumu kwa hatua watakayo ichukua na kuwataka wakuu wa wilaya kusimamia agizo hilo.
“Nimesema msiwe viwanda vya kuzalisha madeni kwa Serikali kutokana na kuwahamisha watumishi bila kuwalipa fedha zao za uhamisho,kama hamna hela za kulipa watumishi msiwahamishe,”amesema.
Aidha amefafanua kuwa kutokana na kitendo hicho cha uhamisho wa watumishi bila kuwalipa imeisababishia Serikali hasara.
Hata hivyo aliwatakakufanya kazi kwa kujituma kwani baadhi ya watumishi waliokutwa na vyeti feki walikuwa wazembe katika utendaji kazi.
“Nimesema msiwe viwanda vya kuzalisha madeni kwa Serikali kutokana na kuwahamisha watumishi bila kuwalipa fedha zao za uhamisho,kama hamna hela za kulipa watumishi msiwahamishe,”amesema.
Aidha alifafanua kuwa kutokana na kitendo hicho cha uhamisho wa watumishi bila kuwalipa imeisababishia Serikali hasara.
Hata hivyo amewataka kufanya kazi kwa kujituma kwani baadhi ya watumishi waliokutwa na vyeti feki walikuwa wazembe katika utendaji kazi.
Mbali na hilo aliwata wakuu wa wilaya kutotumia madaraka yao vibaya ya kuwaweka watumishi ama wananchi ndani bila makosa bali wafuate sheria,kanuni na na taratibu za kazi.