- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : SIMBACHAWENE ATEUWA MADIWANI WAWILI
DODOMA : WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI,GEORGE SIMBA CHAWENE amemteua msomi Profesa George Mwamfupe kuwa diwani wa Manispaa ya Dodoma miongoni mwa madiwani wengine wawili ambao wameteuliwa na Waziri huyo.
Uteuzi huo wa Waziri Simbachawene umefanyika ili kuboresha huduma za kimaendeleo katika mji wa Dodoma kutokana na kuwepo kwa Makao makuu ya Serikali Dodoma ambapo diwani mmoja ametoka CHADEMA na wawili CCM.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri Simbachawene na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma,GODWIN KUNAMBI wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
KUNAMBI amebainisha kuwa uteuzi huo wa Waziri umefanyika baada ya Vyama vya CCM na CHADEMA katika Manispaa hiyo kuyapendekeza majina 6 kwa kuyapigia kura na kuyawasilisha kwa Waziri.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa ya Mamlaka ya Miji sura ya 288 kifungu cha 24 kifungu kidogo cha pili d ya mwaka 2004 na hivyo kufanya idadi ya madiwani wa Manispaa ya Dodoma kufikia 60.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema kuwa watawapimia maeneo wale ambao walivamia muda mrefu na hawajajenga na hawataruhusu ujenzi holela na badala yake watawabomolea nyumba zao wale wote watakaobainika kujenga kiholela.
Pia amewataka wale wote ambao wanataka kujenga nyumba wafike katika Manispaa hiyo ili waweze kupewa kibali.