Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:54 pm

NEWS: SIMBACHAWENE AMWAGIZA DC MARA KUINGILIA KATI MRADI WA KILIMO CHA MIWA

Dodoma: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Geogre Simbachawene amemwagiza mkuu wa mkoa wa Mara Dr. Charles Mlingwa kuingilia kati mradi wa kilimo cha miwa na kiwanda cha kutengeneza sukari ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Waziri huyo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara Apoo Tindwa kuhakikisha mradi wa shamba la miwa pamoja na kiwanda cha sukari unakamilika haraka kama ilivyokusudiwa.

Chawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na Madiwani,Wenyeviti wa vijiji na wajumbe wa halmashauri ya serikali ya vijiji wa wilaya ya Tarime.

Amesema kuwa uwekezaji wa viwanda na kilimo ni agenda kubwa sana katika taifa hivyo basi mradi huo unatakiwa utekelezwe haraka.

Pia ameitaka halmashauri hiyo kuhakikisha inasimamia mikataba ambayo vijiji vinaingia na mwekezaji ili kuweza kuwasaidia kutokudhurumiwa na mwekezaji.

Amesema ameshangazwa na Halmashauri hiyo ndiyo inaingia mkataba na mwekezaji badala ya vijiji hivyo na kuonyesha wazi katika mradi huo siasa ambayo itatendeka.

Naye Diwani wa Kata ya Regicheri halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara JOHN MBUSIRO akisoma taarifa kwa Waziri huyo amesema kuwa wakazi wa wilaya ya Tarime zao lao kubwa lilikuwa ni kilimo cha bangi lakini sasa wameamua wameachana nalo kwasababu limekuwa likiwaathiri vijana pia hata wazee nao wakaingia katika uhuzaji wa bangi.

Amesema kuwa mradi huo ukichelewa wanaweza kuupoteza kwani Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) walikwisha wataadharisha jambo hilo.

Amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Tarime ni wakala wa maendeleo lakini ucheleweshwaji huo unakinzana na dhana ya Halmashauri kuwa wakala wa maendeleo na pia unakinzana na agenda ya Tanzania ya Viwanda.

Hata hivyo vijiji vilivyopitiwa na miradi hiyo ni Bisarwi,Weigita,Matongo na Keisaka kwajili ya kuwezesha upatikanaji wa maeneo ya uwekezaji.