- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHULE YA MSINGI YA MBALAWALA YAPATA NEEMA YA WALIMU
DODOMA: HATIMA ya serikali imetimiza adhima ya kupeleka walimu 10 katika shule ya msingi Mbalawala katika manispaa ya Dodoma iliyokuwa ikikabiliwa na tatizo la upungufu wa walimu kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha wazazi kuifunga na kuuondoka na watoto wao.
Afisa elimu wa manispaa ya Dodoma, Mwisungi Kigosi akizungumza katika mkutano wa wazazi pamoja na wanafunzi wa shule hiyo alisema kuwa idadi hiyo ya walimu itasaidia katika kupunguza changamoto iliyokuwepo awali.
Alisema kuwa kupatikana kwa walimu hao ni jitihada za makusudi zilizofanya kwa kushirikiana na waratibu elimu kata ambao walisaidia katika kuwapata walimu hao ambao wapo tayari kufundusha shule hiyo.
Aidha aliwataka wazazi wa kijiji hicho kutoa ushirikianao kwa walimu hao waliopatikana ili kuweza kuwapa motisha ya kuendelea kufundisha katika shule hiyo kwa muda mrefu.
“Mimi ni mgeni hapa lakini toka nimeletwa hapa nikakabidhiwa jukumu hili la kuwapata walimu hao ambao nimekuja nao leo na nimetumia jitihada kubwa sana kuwapata hivyo basi wazazi mjitahidi kuwapa ushirikiano hawa walimu sio leo tu tunaondoka nasikia wamehama”alisema Kigosi.
Hatahivyo aliwaagiza wazizi hao kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule na kuacha utoro ambao awali walikuwa nasingizia kukosdekana kwa walimu na kuondoa tatizo la kushuka kwa ufaulu.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Moses Risasi alisema kuwa kuongezeka kwa walimu hao kutasaidia kuongeza ufanisi katika kazi zao kutokana awali kulemewa na idadi kubwa ya wanafunzi.
“Kama mwalimu wangu wa darasa la pili alikuwa anafundisha wanafunzi 236 hivyo utaona ni jinsi alikuwa anapata shida unakuta muda mwingine hasahihishi madaftari hata mwezi mzima”alisema Risasi.
Risasi alisema kuwa walimu waliokuwepo ni saba lakini wanafunzi 922 idadi ambayo haiendani lakini kwa ujio wa walimu hao 10 angalau chanamoto hiyo itapungua.
Shule hiyo ambayo ipo ndani ya Manispaa ya Dodoma imekuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu kwa muda mrefu hali ambayo ilisababisha wazazi katika kijiji hicho kuifunga na kuamua kurudi na watoto wao kwa madai kuwa wanapoteza muda.
Mara baada ya wazazi hao kuamua kuifunga shule hiyo na taarifa kulipotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachewene aliitembelea shule hiyo na baadaye alimvua madaraka aliyekuwa afisa elimu Manispaa Schora Kapinga kwa madai ya kutolifanyia kazi tatizo hilo.