Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:22 pm

NEWS: SHULE YA HUZI CHAMWINO YAPATA NEEMA YA MABATI

DODOMA: Kampuni ya kutengeneza mabati ya ALAF imetumia zaidi ya shilingi milioni 200 kwenye miradi mbalimbali ya kijamii nchini ikiwemo mradi wa Malaria, kifua kikuu na ukimwi ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani kwa watanzania ambao wanathamini bidhaa za kampuni hiyo kwa kuzinunua na kuzitumia.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa mabati bando 500 yenye thamani ya shilingi milioni saba kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Huzi iliyopo wilayani Chamwino iliyoezuliwa na upepo mkali hivi hivi karibuni,Meneja wa alaf kanda ya kati bw,Grayson Mwakasege amesema kampuni hiyo imeona umuhimu wa kutoa msaada huo kwa kuwa imekuwa ikishirikiana vema na wananchi wa mkoa wa Dodoma na nchini kwa ujumla hasa kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa jamii ya watanzania wakati huu wa kuelekea uchumi wa viwanda.


Upande wake mbunge wa jimbo la Mtera mh, Livingstone Lusinde ameushukuru uongozi wa alaf kwa ukarimu wao waliouonyesha huku akisema kuwa kuwepo kwa kiwanda hicho mkoani dodoma kumekuwa na manufaa kwa wananchi nakuongeza kuwa shule hiyo ya Huzi ni chakavu na serikali haina uwezo wa kuhudumia shule zote kwa mara moja kutokana na majanga yaliyotokea

Aidha ameongeza kuwa serikali kupitia waziri wa elimu, sayansi na teknolojia prof, Joyce Ndalichako imetoa shilingi milioni 66 kwa ajili ya kujenga madarasa mapya ili kuhakikisha miundombinu ya shule hiyo inarudi katika hali yake ya kawaida na wanafunzi kuendelea na masomo yao kwa haraka