- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI TUCTA LALIA NA MISHAHARA KIDUCHU WAKATI WA MAADHIMISHO YA MEI MOSI
Dodoma: Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TCTA) Mkoa wa Dodoma,kipato cha mshahara kwa mfanyakazi kwa mwezi hakikidhi mahitaji kwa mfanyakazi.
Hayo yameelezwa na Shirikisho hilo wakati Katibu wa TUCT mkoa wa Dodoma Ramadhani Mwendwa wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa awe mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
Hata hivyo Rugimbana alimkaimisha mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabiri Shekimweli.
Katika risala hiyo Mwendwa amesema kipato cha ujira wa mshahara wa mwezi wanacholipwa wafanyakazi hakiridhishi kabisa.
Akizungumzia sekta binafsi Mwendwa alisema sekta hizo zimekuwa bingwa kuwanyonya wafanyakazi wao kwa kutowapatia mikataba ya kazi.
“Sekta binafsi waajiri wamekuwa bingwa wa kuwanyonya wafanyakazi ikiwemo tabia ya kutofuata sheria za Ajira kwa kuajiri wafanyakazi bila kuwapa mikataba ya ajira ili kutimiza dhuruma yao ikiwemo kutowachangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na kukwepa kodi ya malipo ya payee” amesema Mwendwa.
Akizungumzia kuhusu madeni sugu Mwendwa aliitaka serikali kulipa madeni yote sugu kwa kada zote ili kuondoa maumivu ya muda mrefu ambayo inawaumiza wafanya kazi.
Aidha ameitaka serikali kutotumia makosa ya baadhi ya watu walioshindwa kutawala walioshindwa kusimamia majukumua yao ya kiutawala kwa kuwaadhibu watu wasio kuwa na hatia.
Amesema licha ya serikali kutoa punguzo kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9 lakini bado wafanyakazi wanaiomba serikali kupunguza kodi hiyo kwa wafanyakazi wengine kwani punguzo hilo limefanyika kwa wafanyakazi wachache wanaolipwa kima cha chini lakini kodi kubwa hadi asilimia 30 inaendelea kukatwa kwa wafanyakazi wenye mishahara mikubwa kana kwamba wanaadhibiwa kwa kulipwa mishahara mikubwa.
Akijibu risala hiyo mkuu wa wilaya ya Mpwapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana,Jabiri Shekimwel amesema serikali inaandaa utaratibu wa kuboresha mishahara ya watumishi wa Umma baada ya kukamilisha zoezi zima la uhakiki wa vyeti.