Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:51 pm

NEWS: SHIRIKA LA WOWAP KUFANYA MAFUNZO KWA WANAWAKE ZAIDI YA 800.

DODOMA: Shirika lisilo la Kiserikali Nchini Tanzania (WOWAP) linatarajia kufanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake zaidi ya 800 katika halmashauri ya wilaya Dodoma Mjini yenye lengo la kuwapa uelewa juu ya masuala ya uongozi na kuwahamsisha kugombea nafasi mbalimbali kwenye chaguzi zijazo.

Akizungumza wakati wakitambulisha Mradi huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi leo Jijini hapo Mkurungenzi wa Shirika la WOWAP ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalumu Mkoani humo Fatma Hassan Toufiq amesema kuna wanawake wengi nchini wanasifa za kuwa viongozi lakini changamoto kubwa ni kutokuwa na uelewa juu ya masuala hayo na huku akidai kuwa pamoja na serikali inatoa elimu lakini haiwezi kuwafikia wanawake wote.

Akiendelea kuelezea amesema lengo ni kuhakikisha vikwanzo vinavyowakumba wanawake kushindwa kufikia lengo namba tano katika malengo endelevu vinapatiwa ufumbuzi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi amesema changamoto wanazozipata wanawake ndizo zinazowapata watoto,wazee na watu wasiojiweza katika familia.

''Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa shughuli nyingi za kitaifa zimekuwa zikimgandamiza mwanamke, tangu Dunia kuubwa hata kwenye Vitabu vya dini nafasi ya mwanamke bado sana,''amesema Mkuu huyo.

Mbali na hayo amesema atahakikishia anawashughulikia watumishi wa Serikali wanaohusika kuwanunua wadada waojiunza( Machangudoa) kwa kuwa wao ndio chanzo cha biashara hiyo haramu kuendelea.

Pia amesema wanawake wengi bado wanakabiliwa na Changamoto ya Mirathi kuwa wanaonewa wananyanyaswa,wanadhurumiwa na kuomngeza kuwa hata mahakamani Rushwa bado imetawala .