Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:52 am

NEWS: SHIRIKA LA RESTLESS DEVELOPMENT LAWASHANGAA VIJANA.

DODOMA: Mratibu Msaidizi wa Shirika Lisilo la Kiserikali Restless Development Denice Simeo amesema kwa mwaka 2015 hadi 2018 utafiti unaonyesha kuwa fedha ambazo zimekuwa zikitengwa kwaajili ya mikopo ni kubwa kuliko fedha zinazochukuliwa

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Simeo amesema kati ya vijana 6,265 waliohojiwa katika utafiti asilimia 74 kati yao hawana uelewa juu ya fedha hizo.

“kuna kiwango kidogo cha uelewa miongoni mwa vijanajuu ya fedha za maendeleo kutokana na utafiti tulioufanya tumebaini kuwa asilimia 25 ya vijana wote Tanzania wanauelewa wa kina kuhusu fedha hizo wakati asilimia 74 hawana uelewa”amesema

Hata hivyo amesema licha ya kuwepo kwa uelewa mdogo juu ya fedha za maendeleo wamebaini kuwa asilimia 92 ya vijana hawawajibiki kutafuta taarifa juu ya fedha hizo

Pia ameendelea kusema Vijana wengi wameshindwa kujiweka katika mfumo rasmi wa kuwezesha kufikia fedha hizi za maendeleo na utafiti unaonyesha kuwa kati ya vijana 10 ni kijana mmoja ndo yupo kwenye kikundi

“matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa vijana 6,265 waliohojiwa vijana 614 sawa na asilimia 9.8 wapo kwenye vikundi wakati vijana 5,651 sawa na asilimia 90.26wamebainisha kutokuwepo katika vikundi”ameongeza Mratibu huyo.

Ameongeza kuwa wapo vijana waliopata mkopo na katika utafiti unaonyesha kuwa asilimia 14.3 wamewahi kushuhudia fedha za maendeleo wakati asilimia 79.6 ya vijana hawakuwahi kushuhudia na asilimia 6.1 wapo ambao hawajui kabisa.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana wawekeze katika utoaji elimu ili kukuza ufahamu na uelewa kwa vijana .