Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:11 pm

NEWS: SHIRIKA LA RELI LAPATA HASARA YA BILIONI 3

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuwa limepata hasara takribani Shilingi bilioni tatu mara baada ya kusitisha safari zake za reli za Kanda ya Ziwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 27, 2020 na Meneja wa Shirika hilo Bw. Masanja Kadogosa wakati akifanyiwa mahojiano na kituo cha runinga cha AzamTV.

Kadogosa amefafanua kuwa pia shirika hilo limetumia takribani Shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa reli kwenye urejeshwaji wa njia iliyoharibika na Madhara yatokanayo na mvua.

"Tumesitisha Safari za Abiria na Zamizigo kwa siku 20, na reli isipofanya kazi kwa siku moja tunapoteza milioni 120" kwahiyo ni takribani bilioni 3 tumepoteza" amesema Kadogosa