Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:37 am

NEWS: SHIRIKA LA POSTA LAONYESHA UZALENDO LAKUSANYA MILIONI 7 KWA MADENI YA MUDA MREFU

DODOMA: Shirika la postaTanzania limefanikiwa kukusanya madeni ya muda mrefu kutoka kwa taasisi za serikali , mashirika ya umma na sekta binafsi shilingi bilioni 7 na milioni 600.

Hayo yamelezwa na Naibu waziri wa ujenzi , uchukuzi na mawasaliano mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa kikao cha kamati ya bunge ya kudumu ya miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo kilichofanyika mjini Dodoma.