Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:28 pm

NEWS: SHIRIKA LA ACTION AID LASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE

DODOMA: Wanawake nchini wamelipongeza shirika la Action aid kwa kuwajengea uwezo wa kupata elimu hasa wanawake wa vijijini ambayo imewasadia kujiamini katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo haki ya miliki ardhi na kuweza kujikwamu katika sekta ya kilimo.

Hayo yameelezwana na mwenyekiti wa jukwaa la wakulima wanawake wadogowadogo wilaya ya chamwino JANETH WILSONI NYAMAYAHASI wakati wa mkutano wa kitaifa wa jukwaa la wakulima wadogo wadogo Tanzania ambao umefanyika leo mjini hapa amesema shirika la action aid limewasidia akina mama kuweza kujua katiba ya nchi kupata elimu ambayo imewasaidi kujitambua na kuweza kufanya maamuzi katika masuala mbalimbali ya kijamii

Lakini pia Ameongeza kuwa mafanikio waliyopata wanawake wengi ni ,mahusiano mazuri kati ya vijiji na majukwaa yameimarika,vikundi vimepewa elimu mbalimabali pamoja na kujua katiba ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa jukwaa la wilaya ya singida AMINA SAIDI DAFI ameweza kubainisha changamoto ambazo ziawakabili ni pamoja na mtazamo hasi kwa baadhi ya jamii na viongozi,utunzaji wa kumbukumbu wa taarifa za fedha.

Sanjari na hayo lengo kuu la mkutano huu ni kuwapatia fursa wakulima wadogo wadogo wanawake kusukuma na kudai madai kwa kutumia vyombo vya habari,kutoa fursa ya wakulima wadogowadogo kushiriki na kukutana na watunga na watekelezaji wa sera na wadau wengine wa sekta ya kilimo juu ya ushiriki wa wakulima wadogo kwenye mipango na sera.