- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHIBUDA AISIFIA SERIKALI YA MAGUFULI
DODOMA: KATIBU Mkuu wa Chama cha ADA-TADEA naMwenyeki wa Baraza la Vyama chama cha TADEA John Shibuda amewataka watanzani wote kumuunga mkono rais wa awamu ya tano Dk.John Magufuli kwa kuonesha ujasili wa kutekeleza ushauri wa wapinzani kwa kupambana na ufisadi, wizi wa madini,rushwa na mishahara hewa.
Alisema kwa sasa Dk.Magufuli anatekeleza kilio cha siku nyingi ambacho kilikuwa kikitolewa na wanasiasa wa vyama vya upinzani kuhusu wizi wa mali ya Umma, ufisadi,utoroshwaji wa madini, mikataba hewa na mibovu, mishahara hewa na mambo mengine ambayo wapinzania walikuwa wanaona kuwa yanalisababishia taifa hasara.
Kutokana na hali hiyo Shibuda amesema kwa kitendo cha Dk.Magufuli kujitoa muhanga kupambana na watu ambao walikuwa wakitafuana mali za Umma na rasilimali zake kinatakiwa kuungwa mkono na watu wote bila kuwa na kijiba cha roho.
Alisema watanzania wanatakiwa kujenga utamaduni wa kuwasifia na kuwatia moyo viongozi ambao wanafanya kazi zao vuzuri hata kama hayupo katika mlengo wako wa kiitikadi lakini ni muhumu kusifia kazi zinazofanyika kama ninaonekana kuwa na tija kwa jamii na kwa taifa kwa ujumla.
“Watazania wengi wamekuwa na tabia ya kuwaonea kijicho na choyo baadhi ya viongozi wa kisiasa au wa kiserikali wanaofanya kazi zao vizuri badala ya kuwasifia.
“Kitendo cha watanzania kutosifiana au kusema ukweli pale mtu anapofanya vizuri ni kuendelea kujifunga katika vifungo vya utumwa ambao hauwezi kuisha”alisema Shibuda.
Shibuda alisema ni vyema sasa wanasiasa na wale ambao siyo wana siasa wakamuunga mkono Rais Dk.John Magufuli pale anapofanya vizuri hasa anapofanya kazi ngumu ya kupambana na wizi wa Madini, madawa ya Kulevya pamoja na kupambana na mafisadi na wale ambao walikuwa wakipata mishahara hewa.
“Mheshimiwa Rais Dk.John Magufuli tukiri bila kijicho kainusuru nchi kutokuwa ni teja la Umma wa watu wa tabasamu bandia za shangwe ziitwazo wajinga ndio waliwao.
“Tanzania ni ukweli usiopingika wa kwamba serikali ya awamu ya tano inastahili pongezi kwa kukomesha uishi wa kanuni za sheria za nchi kuwa ni taifa la kujinyang’anya na kujidhurumu sisi wenyewe thamani ya manufaa ya rasilimali za maliasili za ardhi ya Jamhuri ya nchi yetu na tumpongeze rais kwa masahihisho ya sheria ya madini.
“Kwa hiyo sasa vyama vyote vya siasa tuache choyo na tuache usengenyaje wa tabia za wivu na husuda za kuacha kuthamini,kusadiki na kupongeza mema ya vipaji na vipawa vya hodari dhahiri za uongozi uitwao maslahi jamii na taifa na anayetakiwa kupongezwa ni Dk.Mgufuli kwa kuwa mkuu wa vita ya kudai ukombozi kwa ustawi wa maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa letu” alisema Shibuda.
Aidha Shibuda alitoa nasaa kwa vyama vyote ya vya siasa vya upinzani kwa kusema kuwa vyama hivyo visibweteke wakati chama tawala kikifanya mageuzi ya kwenda sambamba na mapinduzi ya utumishi wa dola.
“Kwa sasa vyama vya siasa tambueni awamu ya kwanza ya siasa za mfumo wa changamoto za mporomoko wa utiifu na uaminifu na za mumomonyoko wa maadili sasa zimekoma,awamu ya pili ya siasa za demokrasia msingi wake ni ushindani wa siasa za hoja za mapiku ya kuvumbua Ustawi wa Maendeleo ya jamii,Uchumi na Taifa.
“Tanzania tupo katika safari ya serikali ya Rais Dk.Magufuli ya kuingia katika awamu ya pili ya utawala bora wa siasa na Demokrasia ni uwajibikaji wa kushindanisha mitazamo ya utawara bora kwa uchumi wa kujenga taifa” alisema Shibuda.
Aidha kiongozi huyo alisema kwa sasa siasa ni kuondoa madhila ya maisha mabovu ya kudhalilisha uishi wa kila mtanzania.
Akizungumzia umuhimu wa baraza la vyama vya siasa alisema vyama vyote vya siasa vinahitaji kuwa na sare ya werevu wa kuondoa ombwe la sintofahamu ya kuhusu dira ya maendeleo ya taifa.