Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:48 am

NEWS: SHEREHE ZA TRUMP SIKU 100 MADARAKANI (FULL SPEECH)

Washington: Rais wa Marekani Bw. Donald Trump Jana amesherekea siku 100 akiwepo madarakani Ikulu ya White House pamoja na kundi la watu wakimshangiri, ambao ni utaratibu wa unaofanywa na Marais wa marekani kama kigezo cha kujipima kasi ya uongozi wako katika kuwepo madarakani tangu kuingia madarakani.

Katika hafla iliofanyika katika Jimbo la Pennsylvania Trump alianza kwa kusifia mafanikio yake ya mwanzo na kuwashambulia wakosoaji ambao wametoa alama mbaya kwa utawaal wake.

Trump aliliambia kundi la watu waliokusanyika kwamba ndio kwanza anaanza kutimiza ahadi zake za wakati wa kampeni. Ameshambulia mara kwa mara vyombo vya habari alivyosema ,"havina uwezo, visivyokuwa wa kweli" , akisema havikuwa vinasema ukweli juu ya mafanikio ya utawala wake.

"Utawala wangu umekuwa ukileta mafanikio kila siku kwa wananchi wa nchi hii," Trump alisema mjini Harrisburg, Pennsylvania. "Tunatimiza ahadi zetu moja baada ya nyingine, na kwa hakika watu wanafurahi sana juu ya hilo."

Trump aliorodhesha baadhi ya mafanikio yake muhimu , ikiwa ni pamoja na mafanikio ya kuthibitishwa kwa jaji wa mahakama kuu Neil Gorsuch na kusafisha njia kwa ajili ya sheria nyingine nyingi kuhusu mazingira na biashara.

Pia ameorodhesha idhinisho lake kwa bomba la mafuta la Keystone XL na Dakota, akiuwa makubaliano ambayo bado hajaanza ya kibiashara na mataifa ya Asia, na kuimarisha hatua za kiusalama ambazo zimesababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa watu kuvuka mipakani kimagendo katika mpaka wa kusini.