- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MPYA WA CONGO AHUDHURIA RAIS MMOJA TU
Sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi imefanyika Jana Alhamisi, Januari 24 mchana kwenye makao makuu ya ofisi ya rais ambapo Sherehe hizo zimehudhuriwa na Rais mmoja tu uhuru Kenyatta wa Kenya, kati ya marais 17 waliotajwa na wizara ya mambo ya nje ya DRC ambao walitarajiwa kuhudhuiwa.
Tshisekedi anakuwa rais wa tano wa nchi hiyo, lakini wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kidemokrasia.
Katika hotuba yake ya kuapishwa, ambayo ilidumu karibu saa moja na ambapo alipata hitilafu ya kiafya, amekaribisha siku hiyo ya kihistoria.
Amemrithi Joseph Kabila ambaye ameondoka madarakani baada ya kuwa madarakani miaka 17.
Imekuwa mara ya kwanza nchi hiyo kushuhudia mabadiliko ya madaraka kwa amani, kutoka rais mmoja kwenda mwingine, tangu ilipopata uhuru mwaka 1960.
Licha ya kuingia madarakani, Tshisekedi mwenye umri wa miaka 55, anaanza kazi kubwa ya kuongoza nchi hiyo yenye utajiri mkubwa rasimali, lililogawanyika kisiasa.
Katika hotuba yake, rais Tshisekedi ameahidi kuliunganisha taifa hilo na kuhakikisha kuwa amani inarejea lakini pia uchumi unaimarika.
Wakati wa hotuba yake, alilazimika kuikatisha baada ya kuugua ghafla jukwani lakini, baada ya muda mfupi akarejea tena na kuendelea na hotuba yake.
Martin Fayulu, aliyewania urais kupitia muungano wa Lamuka, anaamini kuwa alishinda Uchaguzi huo na hatambui ushindi wa Tshisekedi kwa sababu aliibiwa kura.
Viongozi wa Kanisa Katoliki, walisusia sherehe hizo , kwa kile walichosema kuwa hawaamini kuwa Tshisekedi alishinda Uchaguzi huo.