- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHEIKH WA MKOA ASISITIZA AMANI
DODOMA: WAUMINI wa dini ya kiislamu nchini wametakiwa kuhakikisha wanatunza amani ya nchi pamoja na kuifanya siku ya sikukuu ya Edd El Fitri kuwa sehemu ya kutafakari mambo mema yaliyokuwa yakifanyika kwa kipindi chote cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Rai hiyo imetolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shabani alipokuwa akitoa mawaidha katika ibada ya sikukuu Edd El Fitri iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi Mjini hapa.
Sheikh Shabani amesema waumini wa dini hiyo wanatakiwa kutafakari kwa kina mambo yote ambayo wamejifunza katika mwezi mtukufu wa ramadhani ili kuendeleza mambo yote mazuri ambayo ni mema mbele za Mungu.
Amesema katika siku ya sikukuu waumini wa dini ya kiislamu wanatakiwa kuonesha mfano mzuri kwa jamii na isiwe siku ya kufanya matukio mbalimbali kama vile ujambazi, ulevi na uzinzi na badala yake wahakikishe wanatunza amani ya nchi.
“Siku ya leo isiwe siku ya kufanya matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani, wapo watu ambao wataitumia siku ya leo kufanya maasi mbalimbali kama vile,uzinzi kufanya magomvi, dhuruma, rushwa pamoja na kufanya fujo katika familia.
“Mnachotakiwa kukifanya ndugu zangu Waislamu ni kuhakikisha mnalinda amani ya nchi kwa njia yoyote ili hata watu ambao ni wadini nyingine waweze kuona kuwa kweli mlitunza amani ya nchi, amani katika ndoa amani katika familia na kulitafakari neno la Mungu kwa misingi ya kumpendezesha Mungu” alisema Sheik Shabani.
Kwa upande wake Shekhe Ahmed Zuberi wa msikiti wa Nunge mjini Dodoma amesema kuwa waislamu wanatakiwa kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanasaidiana katika shida la raha.
Amesema kuwa waislamu wengi nchini wamekuwa wakilalamika kila siku kuwa wanaonewa lakini hali hiyo inatokana na wao kutokuwa na mipango ambayo ingewaisaidia katika kuhakikisha kuwa wanapiga hatua kiuchumi.
“Watu wa dini ya mabohola wapo milioni mbili ulimwenguni lakini kutokana na mipango yao mizuri ndiyo maana hata leo wanao uwezo wa kusaidia hata taifa letu, kipindi cha nyuma kiongozi wao alikuja kutoa msaada kwa Rais wetu nah ii kutokana na kuwa na moyo wa kuwa lakini sisi waislamu leo hii ukisema hata tuchangia shilingi elfu moja tu kila mmoja wetu inakuwa tabu”alisema Shekhe Zuberi.
Hata hivyo amewataka waislamu kuendelea kufanya mambo mema ambayo walikuwa wakiyafanya katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani kwa kipindi chote.