- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHAMSIA WAZITAKA TAASISI KUTOA MISADA KWA MAKUTI YA WATU WENYE UHITAJI
DODOMA: Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam mkoa wa Dodoma β SHAMSIA Women Group wamezita Taasisi mbalimbali kutoa misaada kwa makundi ya watu wenye uhitaji.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo NURU JABIRI ametoa rai hiyo wakati wakigawa chakula kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambapo amesema kuwa jamii imekuwa ikiwasahau watu wenye uhitaji ikiwa ni pamoja na wagonjwa.
Amesema kuwa pamoja na kupata dawa lakini bado wagonjwa wanahitaji mahitaji mengine ikiwa ni pamoja na upendo, mavazi na msaada wa chakula.
Kwa upande wake JASMINE AWADHI ambaye ni mkazi wa Dodoma pia ameziomba Taasisi na Mashirika mengine kujitokeza kuunga mkono katika kutoa misaada kama hiyo kwa watu mbalimbali wenye mazingira magumu na hawana watu wa kuwapa mahitaji yanayohitajika.
Baadhi ya wagonjwa waliopatiwa chakula hicho wameishukuru jumuiya hiyo kwa kuona uhitaji wao na kuomba watu wengine wenye uwezo kujitokeza kutoa misaada kama hiyo kwa jamii.