- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHAMBULIZI LA BOMU LAWAUA WATU 24 KABUL
KABUL: Shambulizi la bomu limesababisha karibu vifo vya watu 24 kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul.
Kwa mujibu wa wizara ya ya mambo ya ndani nchini Afghanistan, takriban watu 42 pia walijeruhiwa wakati wa mlipuko huo.
Image caption Shambulizi la bomu lawaua watu 24 Kabul
Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika eneo lenye washia wengi magharibi mwa mji.
Lengo la shambulizi hilo halikutajwa mara moja na hakuna mtu aliyedai kuhusika.
Shambulizi hilo llitokea karibu na nyumba na afisa wa cheo cha juu serikalini, Mohammad Mohaqiq.
Hakuna kundi la kigaidi lililodai kuhusika.
Mashambulizi ya awali yamedaiwa kutekelezwa na Taliban au kundi la Islamic State.
Kabul umekumbwa na misururu ya mashambulizi likiwemo lililowaua watu 90 wakati lori lililipuka mwezi Mei.