Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:33 am

NEWS: SERIKALI YAZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUTENGA ASILIMIA 10 KWA VIJANA NA AKINA MAMA ILI KUJIKWAMUWA NAUMASIKI

Dodoma: Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha inatenga asilimia 10 kwa ajili ya akina mama na vijana ili kujikwamua katika umasikini.

Kauli hiyo imetolewa na Bungeni na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais –TAMISEMI,Selemani Jaffo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge Stanslaus Mabula (CCM).

Akiuliza swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini serikali isiziagize halmashauri zote nchini kutenga asilimia 15 kwa ajili ya vijana na akina mama kulingana na kupanda kwa maisha pamoja na vijana na akina mama kuongezeka.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua kama serikali iko tayari kutoa agizo la msisitizo kwa halmashauri zote nchini kutenga fedha hizo na wala wasichukulie kama hisani.

Akijibu swali hilo Jaffo,alisema halimashauri zote nchini zinatakiwa kutenga fedha hizo kwa ajili ya akina mama na vijana na hisionekane kama vile ni hisani.

Mbali na hilo alisema kwa sasa serikali haiwezi kukubali halmashauri kutenga asilimia 15 kwa ajili vijana na akina mama kutokana na hali halisi ya uchumi ilivyo.

“Halmashauri zote zinatakiwa kutekeleza agizo la kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mfuko wa vijana na wanawake.

“Katika mwaka wa fedha 2016/17 halmashauri zilitenga sh.bilioni 56.8 ambapo hadi machi 2017 kiasi kilichopelekwa kwenye mfuko kilikuwa sh.bilioni 16.05,halmashauri ya Jiji la Mwanza pekee imeishapeleka sh.milioni 147” amesema Jaffo.

“Natoa wito kwa halmashauri zote nchini kwanza kutenga maeneo rafiki ya kufanyia biashara kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo,kupeleka fedha kwenye mifuko na kusimamia marejesho ili ziweze kunufaisha makundi mengine” amesisitiza Jaffo.