Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:48 pm

NEWS: SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUONDOA KODI ZA UVUVI

DODOMA: SERIKALI imesema imeweka mikakati ya kuondoa kodi katika zana za Malighafi za uvuvi zikiwemo injini za kupachikia nyuzi za kushonea nyavu na vifungashio.

Hayo yameelezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Mhe. William Ole Nasha wakati akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Pangani,Jumaa Hamidu Aweso(CCM)aliyetaka kuju serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wavuvi wa Pangani mitaji na vitendea kazi licha ya Wilaya ya Pangani kuwa na Bahari ya Hindi lakini wavuvi wa Wilaya hiyo hawajanufaika ipasavyo.

Akijibu swali hilo Ole Nasha amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya uvuvi nchini yenye lengo la kuendeleza wavuvi nchini wakiwemo wavuvi wa Wilaya ya Pangani ili waweze kupata ajira.

Hata hivyo amebainisha kuwa Serikali imewawezesha wavuvi wa uvuvi endelevu wa Pweza.